Tovuti static ni chaguo zuri pale biashara inapohitaji uwepo wa haraka na wazi mtandaoni. Inafaa kwa wasifu wa kampuni, portfolio, kurasa za matangazo na kurasa za huduma ambazo hazibadiliki kila wiki. Mara nyingi tovuti static ni rahisi kuitunza, hupakia haraka na gharama yake ni nafuu kwa timu ndogo.

Tovuti dynamic ni bora pale biashara inapohitaji dashboard, kuchapisha blogu, akaunti za watumiaji, masasisho ya bidhaa, mfumo wa booking au mabadiliko ya maudhui mara kwa mara. Inampa timu udhibiti zaidi, lakini inahitaji mipango zaidi kuhusu usalama, hosting, backup na usimamizi wa maudhui.

Uamuzi mzuri huanza na mtiririko wa kazi, si teknolojia pekee. Uliza nani atasasisha tovuti, masasisho yatafanyika mara ngapi, wateja wanahitaji kufanya nini mtandaoni na kama biashara itaongeza vipengele baadaye. Mshirika mzuri wa teknolojia anapaswa kukusaidia kuchagua njia rahisi zaidi inayoweza kukua na biashara.